MD TWANGE ATOA RAI KWA MAMENEJA TANESCO KUONGEZA KASI YA KUPAMBANA NA WIZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME
MD TWANGE ATOA RAI KWA MAMENEJA TANESCO KUONGEZA KASI YA KUPAMBANA NA WIZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME *Afungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mameneja na Wakurugenzi wa Kanda, Dodoma *Asisitiza umuhimu wa kuongeza ubunifu katika ukusanyaji wa mapato *Awapongeza kwa kazi nzuri na kuendelea kuimarisha mahusiano na wadau Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, ametoa rai kwa mameneja wa TANESCO nchini kusimamia na kupambana kwa nguvu zote na changamoto ya wizi wa miundombinu ya umeme, ambayo imekuwa ikijitokeza katika maeneo mbalimbali ya mikoa wanayoisimamia. Bw. Twange ameyasema hayo Juni 24, 2026, mkoani Dodoma wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa Mameneja na Wakurugenzi wa Kanda, wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Shirika pamoja na Kurugenzi ya Usambazaji. Licha ya kuwapongeza mameneja hao kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuwahudumia wananchi, amesema kuna haja ya kila mmoja kuona uchungu wa mali za Shirika kwa kuongeza jitihada za kuhakikisha changamoto ya wizi wa miundombinu ya umeme inatokomezwa. “Nawapongeza kwa kazi nzuri mnay…