MAFINGA YAASWA KUFUNGA HOJA ZA CAG, KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WAZEMBE
MAFINGA YAASWA KUFUNGA HOJA ZA CAG, KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WAZEMBE NA DENIS MLOWE, MAFINGA – IRINGA MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ameziagiza halmashauri kuhakikisha zinachukua hatua za haraka kutekeleza mapendekezo ya wakaguzi wa ndani ya Sekretarieti ya Mkoa (SEA) pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akionya kuwa kupuuza ushauri huo husababisha maagizo mazito na kuendelea kujirudia kwa hoja za ukaguzi. Akizungumza katika Baraza Maalumu la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Mafinga lililokutana kujadili hoja za ukaguzi wa CAG, Kheri alisema ushauri wa wakaguzi unapaswa kufanyiwa kazi mapema ili kuzuia halmashauri kuingia kwenye wakati mgumu wa kujieleza mbele ya Kamati za Bunge za Usimamizi wa Hesabu za Serikali. Alieleza kuwa kujirudia kwa hoja zilezile kila mwaka ni dalili ya kutokuzingatia ushauri unaotolewa na mamlaka za ukaguzi, jambo linaloathiri taswira ya halmashauri na kuongeza mzigo wa uwajibikaji kwa viongozi na watendaji. Mbali na kusisitiza nidhamu katika usimamizi wa fedha za umma James alizitaka halmashauri kuo…