KUNDI C LAFUKUTA ‘MOTO’ BRAZIL, MOROCCO NA SCOTLAND ZATAFUTA NJIA ZA KUFUZU

KUNDI C LAFUKUTA ‘MOTO’ BRAZIL, MOROCCO NA SCOTLAND ZATAFUTA NJIA ZA KUFUZU
NA MWANDISHI WETU, NOEL RUKANUGA Katika michuano ya Kombe la Dunia 2026, huenda hakuna kundi lililoibua mvuto mkubwa kama Kundi C. Baada ya kila timu kucheza mechi mbili, Brazil na Morocco zina pointi nne kila moja, Scotland ina pointi tatu, huku Haiti ikisalia bila pointi. Kwa mtazamo wa haraka, unaweza kudhani Brazil na Morocco tayari zimeweka mguu mmoja katika hatua ya 32 Bora. Hata hivyo, ukiangalia kwa undani zaidi, utaona kuwa hakuna timu iliyojihakikishia kufuzu. Ili ni kundi lenye simulizi nyingi kwa wakati mmoja. Brazil inapambana kurejesha hadhi yake ya kuwa miongoni mwa mataifa makubwa ya soka duniani. Morocco inataka kuthibitisha kuwa mafanikio yake ya miaka ya karibuni hayakuwa ya bahati nasibu. Scotland inatafuta kurejea katika ramani ya soka la dunia, huku Haiti, licha ya kupoteza mechi zake zote mbili, bado ikiwa na uwezo wa kuathiri hatima ya wapinzani wake. Kilichoongeza mvuto wa kundi hili ni kwamba hakuna timu iliyoonyesha ubabe wa wazi dhidi ya washindani wote baada y…