KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 , TRA YAFANYA KONGAMANO LA MAADILI NA VIONGOZI WA DINI

KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 , TRA YAFANYA KONGAMANO LA MAADILI NA VIONGOZI WA DINI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupitia Idara ya Mambo ya Ndani (INAD), leo Juni 17, 2026 imeandaa Kongamano la Maadili lililowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali kujadili nafasi ya maadili katika kuimarisha ukusanyaji wa kodi na kujenga utamaduni wa ulipaji kodi kwa hiari. Kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Miaka 30 ya TRA yatakayofanyika Julai 1, 2026. Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA, Naibu Kamishna wa TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha, amesema kuwa katika kipindi cha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa TRA, taasisi hiyo imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato, huku maadili yakiendelea kuwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yake. Bw. Mcha amesema TRA inaendelea kuwekeza katika mifumo na mikakati mbalimbali ya kuimarisha maadili kwa watumishi wake na walipakodi ili kujenga uaminifu, uwajibikaji na kuongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa hiari. “Maadili hujenga imani, na imani hujenga ulipaji wa kodi kwa hiari,”…