HALMASHAURI YA KISHAPU YAPOKEA MPANGO KAZI WA JAMII WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI KUPUITIA PROGRAMU YA SCALE
HALMASHAURI YA KISHAPU YAPOKEA MPANGO KAZI WA JAMII WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI KUPUITIA PROGRAMU YA SCALE
Na Sumai Salum- Kishapu Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani shinyanga imepokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) utakaotekelezwa katika Kata 10 kati ya 29 za Halmashauri hiyo kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Nation Program - SCALE), inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026 hadi 2029/2030. Akiwasilisha mpango huo katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mratibu wa Programu ya SCALE, Revosatus Mboya, amesema programu hiyo inalenga kuongeza uwezo wa serikali za mitaa na jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia utekelezaji wa miradi inayotokana na mahitaji halisi ya wananchi. Amesema Halmashauri imepokea hadi sasa jumla ya TSh milioni 74,496,045.70 kutoka Benki ya Dunia, fedha ambazo zimet…