EACOP YACHOCHEA AJIRA,UCHUMI NA MAENDELEO TANGA
Na Oscar Assenga, Tanga WAZIRI wa Nishati, Dkt. Deogratius Ndejembi, amesema ujenzi wa Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umefikia asilimia 86, huku mafuta ya kwanza yakitarajiwa kupokelewa katika Kituo cha Chongoleani, Tanga, na kusafirishwa Januari mwaka 2027. Dkt. Ndejembi alisema hayo leo baada ya kutembelea eneo la mradi Chongoleani, mkoani Tanga, kujionea maendeleo ya utekelezaji wake, ambapo alieleza kuwa matarajio ni kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwisho wa Agosti mwaka huu. Alisema kazi nyingi muhimu zimekamilika na kilichobaki ni hatua za mwisho ikiwemo kukamilisha miundombinu ya umeme ili kuwezesha mitambo ya kusukuma mafuta kufanya kazi. "Nimefurahishwa na maendeleo ya mradi. Kazi kubwa imefanyika na tunaamini ifikapo mwisho wa Agosti ujenzi utakuwa umekamilika. Ratiba inaonyesha kuwa meli ya kwanza itachukua mafuta ghafi kutoka Chongoleani mwezi Januari, 2027," alisema. Hata hivyo, alisema changamoto iliyobaki ni kukamilika kwa nj…