WAFANYAKAZI BENKI YA CRDB WAPIMA AFYA, WASHIRIKI MICHEZO KUIMARISHA UFANISI WA KAZI
WAFANYAKAZI BENKI YA CRDB WAPIMA AFYA, WASHIRIKI MICHEZO KUIMARISHA UFANISI WA KAZI
Na Marco Maduhu, SHINYANGA WATUMISHI wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wamepima afya na kushiriki michezo mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya Wellness Day, tukio lililolenga kuimarisha afya ya akili na mwili ili kuongeza ufanisi kazini na utoaji wa huduma bora kwa wateja. Tukio hilo limefanyika Mei 2, 2026 katika viwanja vya michezo vya Fresho vilivyopo Manispaa ya Shinyanga, likiwakutanisha watumishi wa benki hiyo katika shughuli za michezo na elimu ya afya. Mmoja wa watumishi hao, Donard Mgaya, amesema tukio hilo limewasaidia kujumuika pamoja, kujuana na kuchangamsha miili, hali inayowapa nguvu mpya ya kuendelea kuwahudumia wateja kwa ufanisi zaidi. “Wellness Day imetusaidia kukutana kama timu, kuimarisha afya zetu na kupata nguvu mpya ya kuwahudumia wateja kwa ufanisi zaidi,” amesema Mgaya. Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana, amesema michezo ina mchango mkubwa katika kuleta furaha kwa watumishi na kuongeza ufanisi kazini, huku akiishukuru benki hiyo kwa kuendelea ku…