KOCHA BINGWA WA MICHEZO YA UOGELEAJI AUSTIN PILLADO ATUA DAR, KUWEKA KAMBI SIKU 10
KOCHA BINGWA WA MICHEZO YA UOGELEAJI AUSTIN PILLADO ATUA DAR, KUWEKA KAMBI SIKU 10
KOCHA BINGWA WA MICHEZO YA UOGELEAJI AUSTIN PILLADO ATUA DAR, KUWEKA KAMBI SIKU 10 Na Mwandishi Wetu Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam HATIMAYE Kocha maarufu kutoka Marekani, Austin Pillado ambaye pia ni Naibu Kocha Mkuu wa timu ya kuogelea kutoka Chuo Washington State, ametua nchini jana Jumapili kwa ajili ya kuendesha kambi maalumu ya mafunzo ya kuogelea kwa muda wa siku 10. Kambi hiyo inayofanyika jijini Dar es Salaam, imeandaliwa na Shule ya Kimataifa ya Monti kwa kushirikiana na Chama cha Mchezo wa Kuogelea Nchini (TSA). Akizungumza na waandishi wa habari katika mapokezi ya kocha huyo kwenye uwanja wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu na Mwanzilishi wa shule hiyo ya Monti International, Fatma Fernandes alisema lengo kuu ni kuinua viwango vya vipaji vya ndani kufikia hadhi ya kimataifa. “Hii ni siku ambayo tunaanza hatua muhimu ya kuinua michezo ya kuogelea na maendeleo ya vijana hapa nchini Tanzania. “Kwa sababu mpango huu wa mafunzo ya…