ALUMNI CBE WATAJWA NGUZO YA KUUNGANISHA ELIMU NA SOKO LA AJIRA
ALUMNI CBE WATAJWA NGUZO YA KUUNGANISHA ELIMU NA SOKO LA AJIRA Na.Sophia Kingimali. Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wametajwa kuwa kiungo muhimu kinachoweza kuziba pengo kati ya elimu ya darasani na mahitaji halisi ya soko la ajira, hatua itakayosaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa. Akizungumza katika hafla ya Alumni Breakfast iliyofanyika leo Mei 4,2026 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, amesema ushiriki wa alumni unaweza kuwa chachu ya mafanikio kwa wanafunzi kwa kuwapatia uzoefu wa vitendo, mafunzo na hata fursa za ajira. Amesema kupitia mitandao ya wahitimu, wanafunzi wanaweza kupata mwongozo sahihi wa taaluma na mahitaji ya soko, jambo linalosaidia kuwaandaa vizuri zaidi wanapohitimu masomo yao. Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Mwalimu Nyerere Kibaha, Profesa Marcellina Chijoriga, amesema alumni wana nafasi ya kipekee ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa kutumia taaluma na uzoefu wao. Amesisitiza kuwa maendeleo ya taifa yanahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali, huku akiwataja wahiti…