WAZIRI MASOUD ATEMBELEA NA KUOMBA DUA KABURI LA MAREHEMU SHEIKH ABOUD JUMBE MWINYI MIGOMBANI

WAZIRI MASOUD ATEMBELEA NA KUOMBA DUA KABURI LA MAREHEMU SHEIKH ABOUD JUMBE MWINYI MIGOMBANI
Na Miza Kona, Maelezo Zanzibar Waziri Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Masoud Ali Mohamed amesema waasisi wa Mapinduzi wamepigania na kuikomboa nchi ili kujenga misingi ya haki na kuietea maendeleo wazanzibari waweze kujitawala. Ameyasema hayo Migombani wakati alipotembelea kaburi na kumwombea dua Marehemu Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi aliyekuwa Rais wa awamu ya Pili wa Zanzibar, amesema viongozi hao wamefanya juhudi kubwa ya kupambana na kuikomboa nchi na kuleta mafanukio na kuwa sadaka kwa kizazi cha sasa na baadae. Amesema wazanzibari wameondokana na unyanyasaji kutokana na mchango wa waasisi hao kuamua kupigana kwa hali na mali kuikomboa nchi ili wananchi wa Zanzibar kupata haki zao ambazo walinyang’anywa na wakoloni na kukosa kuzitumia. “Viongozi wetu hawa walipambana kuigombania nchi katika kujenga misingi ya haki na kujenga nchi yao kwa nguvu zao zote ili kihakilisha kuwa wazanzibari wanapata haki zao na kuweza kujitawala wenyewe” amefahamisha Waziri Masoud. Aidha amefahamisha kuwa Serikal…