WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGIA BILIONI 25 KUJENGA KITUO CHA MOYO KCMC

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGIA BILIONI 25 KUJENGA KITUO CHA MOYO KCMC
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) Profesa Gileard Masenga akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 9, 2026 jijini Dar es Salaam (PICHA NA NOEL RUKANUGA) Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto kutoka KCMC Dkt. Ronald Mbwasi akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 9, 2026 jijini Dar es Salaam. ………….. NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) imetoa wito kwa Watanzania kushiriki katika uchangiaji wa ujenzi wa jengo la huduma za matibabu ya moyo. Kiasi cha shilingi bilioni 25 kinahitajika kukamilisha mradi huo. Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 9, 2026 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Profesa Gileard Masenga, amesema gharama za ujenzi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba na vifaa vya hospitali zinakadiriwa kufikia jumla ya shilingi bilioni 25. Ameeleza kuwa wataalamu watakaohudumia kitengo hicho tayari wamepata mafunzo ndani na nje ya nch…