TANZANIA SI KISIWA, TAKWIMU ZA MAFUTA GHAFI DUNIANI ZINAJIELEZA!

Tanzania si kisiwa. Takwimu za S&P Global Platts (Aprili 2026) zinaonyesha Bei ya Mafuta Ghafi Duniani imepanda kwa 88% ndani ya Mwezi Mmoja kutokana na Mzozo wa Mashariki ya Kati. Wakati Soko la Dunia likipanda Kwa Kiwango hicho, Bei ya ndani ya Tanzania imepanda kwa 33% tu. Hii inamaanisha Serikali imevunja Makali ya Bei kwa “kubeba” (Absorb) zaidi ya Nusu ya Pigo la Dunia ili Kumlinda Mwananchi. Hatulaumu Mawimbi, tunampongeza Nahodha kwa kuimudu Meli! Ukitaka kujua ufanisi wa Serikali, tazama Majirani. Mfumo wetu wa Uagizaji wa Pamoja (Bulk Procurement) umetuepusha na Madalali ambao wangeongeza zaidi ya Sh 500 kwa kila lita. Ulinganifu wa Bei (Makadirio ya Aprili 2026 kwa Lita/Tsh): ✓Malawi: Sh 4,500+ ✓Kenya: Sh 4,150+ ✓Uganda: Sh 4,200+ ✓Tanzania: Sh 3,800 Tanzania bado ina Bei tulivu na ya Ushindani zaidi Ukanda huu. Huu ndio Upendo wa Serikali kwa vitendo, si kwa Maneno! Ni rahisi kusema “Futa kodi Zote,” lakini takwimu hazidanganyi. Ndani ya kila lita ya Mafuta, kuna Fedha inayokw…