SIMBA YABANWA NA TRA UNITED, MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU
Simba SC imeshindwa kupunguza pointi dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, baada ya kubanwa mbavu ya kutoka sare tasa na TRA United, katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa leo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Kufatia matokeo hayo imeifanya Yanga kuzidi kukaa kileleni wakiwa na pointi 44, ikiwaacha wekundu hao wa Msimbazi wakiwa na pointi 36 ikikamata nafasi ya pili. Katika mchezo huo Simba ilianza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikijaribu kusaka bao la mapema, lakini TRA United ilionekana kuwa bora katika kulinda ikiongozwa na nahodha, Nassry Kombo huku ikitumia idadi kubwa ya viungo, akiwemo Jamali Dulazi, Chanda Chewe na Ally Ng’anzi kudhibiti presha ya mshambulizi ya wekundu hao wa Msimbazi. Kocha wa TRA United, Etienne Ndayiragije, alionekana kuingia na mpango mzuri ambapo wachezaji wake waliongeza presha ya kutafuta mpira mara tu wanaposogea katika nusu ya pili ya uwanja kwa kutumia muundo ya pembe tatu. Tofauti na ilivyokuwa katika mechi tano zilizopit…