SABA WAKAMATWA, WAWILI WAKIHUKUMIWA MIEZI SITA JELA KWA MADAI YA KUIBIWA NYETI ZAO

SABA WAKAMATWA, WAWILI WAKIHUKUMIWA MIEZI SITA JELA KWA MADAI YA KUIBIWA NYETI ZAO
Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa leo Jumatano Aprili 08, 2026 limetangaza kuwakamata Vijana saba katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, wawili kati yao wakipandishwa Mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela kila mmoja, kwa kudai kuibiwa nyeti zao suala ambalo si kweli na lilichochea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwashambulia watu wasiokuwa na hatia. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Shadrack Masija amewaambia waandishi wa habari kuwa hatua hiyo imetokana na msako uliofanywa Aprili 06, 2026 kufuatia taharuki zilizosababisha vurugu na kukosekana kwa amani na utulivu wa jamii katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mkoani Rukwa kutokana na baadhi ya watu kudai kuibiwa nyeti zao. "Vijana wawili kati ya saba ambao ni Haruni Willium Mengo (24) Mkazi wa Kalambazile na Isack Simon Kaniki (19) mkazi wa Mshani wamefikishwa mahakamani na kuonekana na hatia na wote wawili wamepewa adhabu ya kutumikia kifungo cha …