ROTARY CLUB YA DAR ES SALAAM YAFADHILI SEMINA YA MBINU ZA ELIMU JUMUISHI
ROTARY CLUB YA DAR ES SALAAM YAFADHILI SEMINA YA MBINU ZA ELIMU JUMUISHI Ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuimarisha elimu bora na kuwawezesha waalimu, Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam kupitia mradi wake wa Gift of education, imedhamini semina ya kuwajengea waalimu wa shule za msingi za manispaa ya Kinondoni uwezo wa mbinu za mafunzo jumuishi. Semina hiyo ya siku mbili iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kinondoni hivi karibuni na kuhudhuriwa na walimu 84 kutoka shule za serikali katika manispaa hiyo iliandaliwa mahsusi ili kuwapa walimu mbinu za vitendo, ili kuongeza ushiriki wa darasani, kukuza mafunzo jumuishi, na kusaidia wanafunzi wenye mahitaji mbalimbali. Semina hiyo ilihusisha mihadhara shirikishi, mijadala ya vikundi na mafunzo kwa vitendo yaliyotolewa na wataalamu wa udhibiti ubora wa manispaa ya KinondoniAkizungumza katika kilele cha mafunzo hayo, Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni anayeshughulikia elimu ya msingi Deograsia Mapunda alisema semina hiyo imekuja wakati muafaka kwani ni kweli walimu wanahitaji kupigwa msasa kuhusu mbinu za mafunz…