MBUNGE NGAJILO AWAFARIJI WAGONJWA HOSPITALINI

MBUNGE NGAJILO AWAFARIJI WAGONJWA HOSPITALINI
NA DENIS MLOWE, IRINGA MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini Fadhil Ngajilo ameungana na waumini wa dini mbalimbali katika kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka kwa kutembelea wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, ikiwa ni jitihada za kuonesha upendo, mshikamano na faraja kwa jamii yake. Katika ziara hiyo, Mbunge Ngajilo alipata fursa ya kuzungumza na wagonjwa pamoja na ndugu zao, akiwatia moyo na kuwatakia uponyaji wa haraka.  Alisisitiza kuwa kipindi cha ugonjwa ni changamoto kubwa kiakili na kimwili, hivyo ni jukumu la jamii kuendelea kuwapa faraja wale wanaokabiliwa na hali ngumu za kiafya. Akiwa wodini, mbunge huyo alikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula, vifaa vya usafi na bidhaa nyingine muhimu kwa baadhi ya wagonjwa. Alisema hatua hiyo ni sehemu ya kumuenzi Kristo kupitia matendo ya huruma yanayoakisi thamani ya Pasaka. “Pasaka ni kipindi cha kutafakari na kukumbushana umuhimu wa upendo, huruma na kuwasaidia wanaohitaji. Wagonjwa ni sehemu ya jamii yet…