AFISA USAFIRISHAJI SIMANJIRO KORTINI KWA WIZI
Na Mwandishi wetu, Simanjiro Afisa usafirishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Ismail Khalifan amefikishwa mahakamani kwa kosa la jinai la wizi wa shilingi 500,000 akiwa mtumishi wa umma. Afisa usafirishaji huyo Ismail amefikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya Simanjiro na kusomewa shitaka hilo la wizi wa shilingi 500,000 fedha ambazo ni mali ya Halmashauri hiyo. Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) Faustin Mushi amesoma shataka hilo Aprili mosi, 2026 mbele ya hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro Charles Uisso. Mushi amesema Ismail anashtakiwa kwa kosa la wizi akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258 (1), 265 na 270 vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 R:E 2023. Amesema Ismail anashitakiwa kwa kosa la wizi wa shilingi 500,000 alizopewa na mwajiri wake kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya magari ya halmashauri ya wilaya hiyo. Amesema katika kesi hiyo ya jinai namba 7118/2026 mshtakiwa alipewa fed…