WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira, Leo Machi 27, 2026, Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi za CCM Wilaya ya Bunda ambazo zilichomwa moto katika na vurugu za Oktoba 29, 2025. Na Mwandishi Wetu. MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewaonya wanachama walioanza harakati za kusaka urais mwaka 2030 kwa kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujawadia, hivyo wanaofanya hivyo wanakiuka kanuni, miongozo na utaratibu. Amesema kuanza mapema harakati za kusaka uongozi kabla ya wakati inaweza kukigawa Chama badala ya kukijenga hivyo inapaswa kukemewa. Wasira alieleza hayo Leo Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi za CCM Wilaya ya Bunda ambazo zilichomwa moto katika na vurugu za Oktoba 29, 2025. Alisema ndani ya Chama kuna kundi la wanachama ambao hawana kazi za msingi ndani ya CCM zaidi ya kujihusisha na makundi ya kisiasa. Kwa muj…