WANAMICHEZO TANGA WATAKIWA KUDUMISHA NIDHAMU ,KUJIANDAA NA UMITASHUMTA TAIFA 2026
WANAMICHEZO TANGA WATAKIWA KUDUMISHA NIDHAMU ,KUJIANDAA NA UMITASHUMTA TAIFA 2026
Na Emma Kigombe Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Tanga, Mwalimu Joseph Shayo, amewataka wanamichezo wote walioshiriki mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa kuendelea kudumisha nidhamu na kuongeza juhudi katika mazoezi ili kujiimarisha zaidi. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya mkoa, Mwalimu Shayo alisema ni muhimu kwa wanamichezo hao kuendelea kufanya mazoezi kwa bidii ili waweze kuwa katika kiwango bora kitakachowawezesha kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo. Alieleza kuwa kambi ya maandalizi kwa wanamichezo waliochaguliwa inatarajiwa kuanza tarehe 25 Mei hadi 5 Juni 2026, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya kitaifa ya UMITASHUMTA. Hata hivyo, alibainisha kuwa bado kutakuwa na mchujo zaidi katika ngazi ya mkoa ili kupata timu bora zaidi itakayoiwakilisha Tanga. “Msibweteke, endeleeni kufanya mazoezi ya kutosha. Tunahitaji timu imara itakayoweza kushindana na kufanya vizuri katika ngazi ya taifa,” alisisitiza. Kwa upande mwingine, Mwalimu Shayo aliwat…