TRA YAANZA KUCHUKUA HATUA UTARATIBU MPYA UINGIZAJI MAFUTA YA KULA

TRA YAANZA KUCHUKUA HATUA UTARATIBU MPYA UINGIZAJI MAFUTA YA KULA
KAMISHINA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Yusuph Mwenda amesema Mamlaka hiyo tayari imeanza kuchukua hatua kuelekea kuanza kutumika kwa utaratibu mpya wa kuingiza mafuta ya kula Tanzania Bara kutoka Zanzibar. Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Machi 24.2026 jijini Dar es Salaam Mwenda amesema miongoni mwa hatua zilizoanza kuchukuliwa ni pamoja na kuunda kamati ndogo ya wataalam inayohusisha Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko, maofisa wa Forodha na waagizaji wa mafuta kwaajili ya kuweka utaratibu utakaoanza kutumika kuingiza mafuta hayo hivi karibuni. Amesema utaratibu huo mpya unalenga kuwezesha biashara ya Mafuta baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na kuchangamsha biashara katika Bandari za Bagamoyo, Mbweni na Kunduchi ambazo ndiyo hutumika kuingiza mafuta hayo. "Tutatoa punguzo kwa mafuta yanayoingia Tanzania Bara kutoka Zanzibar ili kuwawezesha wanaoingiza mafuta hayo kupata faida, Serikali kupat…