Serikali Yaweka Mkazo Kuboresha Uwekezaji Kufikia Uchumi wa Kipato cha Juu 2050

Serikali Yaweka Mkazo Kuboresha Uwekezaji Kufikia Uchumi wa Kipato cha Juu 2050
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza leo Machi 27, 2026 jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Uhakiki wa Rasimu ya Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II). Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, akizungumza leo Machi 27, 2026 jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Uhakiki wa Rasimu ya Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II). Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI) umeendelea kuwa nyenzo muhimu katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini, hatua inayochochea ukuaji wa uchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje. Dk. Mwinyi ameyasema hayo Machi 27, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Mkutano wa Uhakiki wa Rasimu ya Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji …