SERIKALI YATOA TRILIONI 1.319 KUIMARISHA MIUNDOMBINU, ULEGA AELEZA MAFANIKIO SEKTA YA UJENZI

SERIKALI YATOA TRILIONI 1.319 KUIMARISHA MIUNDOMBINU, ULEGA AELEZA MAFANIKIO SEKTA YA UJENZI
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuwa Serikali imeendelea kupiga hatua katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo hadi kufikia Machi 2026 jumla ya shilingi trilioni 1.319 tayari zimetolewa kwa ajili ya miradi iliyoidhinishwa katika mwaka wa fedha 2025/2026. Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na makadirio ya mwaka 2026/2027 kwa fungu 98 la Wizara ya Ujenzi, leo Machi 23, 2026 Mkoani Dodoma, Ulega alieleza fedha hizo ni sawa na asilimia 72.80 ya bajeti iliyoidhinishwa na kubainisha mafanikio yaliyopatikana hadi kufikia Machi, 2026. Ulega ameeleza katika Sekta ya barabara, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kilometa 206.33 za barabara kwa kiwango cha lami pamoja na madaraja makubwa manne. Aidha, miradi 76 kati ya 81 ya dharura ya ujenzi wa madaraja yaliyoathiriwa na mvua za El-Nino imekamilika. Ulega alibainisha kuwa ujenzi wa madaraja muh…