SERIKALI YATOA BILIONI SITA KUKABILI POLIO KWA WATOTO MILIONI SITA KWA MIKOA SABA
SERIKALI YATOA BILIONI SITA KUKABILI POLIO KWA WATOTO MILIONI SITA KWA MIKOA SABA Na Hassan Kimweri, WAF – Mwanza Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni Sita kwa ajili ya chanjo ya polio ya matone itakayotolewa kwa watoto milioni Sita chini ya miaka 10 kwa mikoa Saba ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora, Singida pamoja na Mara. Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela amesema hayo leo Machi 24, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akimuwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya polio ya matone mkoani Mwanza. “Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu huu na kutoa fedha hizo, zaidi ya miaka 30 Tanzania haina ugonjwa huu lakini zipo nchi jirani bado ugonjwa huu upo, chanjo yetu hii inaandaa watoto wetu ili waweze kuimarisha kinga zao na kukabiliana na ugonjwa huu wa polio,” amesema Mhe. Shigela Aidha, Mhe. Shigela amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa timu zitakazozunguka katika mikoa hiyo ili watoto chini ya miaka 10 wapate chanjo ya polio kwa aw…