OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAWASILISHA TAARIFA YA BAJETI

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAWASILISHA TAARIFA YA BAJETI
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Jackson Kiswaga wameridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais ambao umechangia maendeleo endelevu. Hayo yamejiri wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2025/26 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira. Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mhe. Kiswaga alisema kuwa kamati hiyo inapongeza Ofisi hiyo kwa kuibadili jamii kuachana na vitendo vya uharibifu wa mazingira kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa katika baadhi ya maeneo nchini. Alisema kuwa kuna mabadiliko makubwa katika maeneo mengi nchini hususan ambayo miradi ya mazingira inatekelezwa kwani inawawezesha wananchi kuacha kukata miti na kuhifadhi misitu na kufanya shughuli za kujipatia kipato bila kuathiri mazingira. “Tunawapongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kazi nzuri pamoja n…