MRADI WA ENGAGE WACHOCHEA MABADILIKO, KUINUA UONGOZI WA WANAWAKE DUNIANI
MRADI WA ENGAGE WACHOCHEA MABADILIKO, KUINUA UONGOZI WA WANAWAKE DUNIANI
Mradi wa uwezeshaji wanawake na jamii kwa ujumla wa 'Engage' umetajwa kuwa chachu muhimu ya mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa wanawake katika mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania. Hayo yameelezwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Engage uliofanyika katika ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam, ukihitimisha mzunguko wa utekelezaji wa mradi huo wa zaidi ya miaka sita. Akizungumza kando ya mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali, amesema mradi huo umeongeza kwa kiasi kikubwa ushiriki wa wanawake katika maamuzi na kuimarisha uongozi wao katika jamii. Amesema kupitia mbinu bunifu na shirikishi, wanawake wamewezeshwa kujitambua, kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii na kuchangia maendeleo ya kiuchumi katika ngazi ya familia na taifa kwa ujumla. Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali, Akizungumza kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Engage uliofanyika katika ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam. Aidha…