WIZARA YA AFYA YAANZISHA MJADALA WA WAZI WA ELIMU YA AFYA KUPITIA TIKTOK LIVE KUWAFIKIA VIJANA WA GENZ.
Na.Elimu ya Afya kwa Umma. Katika kuhakikisha Elimu ya Afya inayafikia kwa urahisi makundi mbalimbali ya Kijamii hususan kundi la vijana wa kisasa ari maarufu Genz, Wizara ya Afya Afya kupitia Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma imeanzisha Mjadala wa Wazi kupitia mtandao wa Kijamii wa Tiktok wa Elimu ya Afya. Akizungumzia kuhusu umuhimu wa mjadala huo unaojulikana kwa jina la Tukutane Tiktok Live, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt.Ona Machangu amesema kupitia mjadala huo utasaidia kwa kasi kubwa vijana kupata taarifa na elimu sahihi kuhusu masuala mbalimbali ya elimu ya Afya kwa vijana wa kizazi cha kidijitali ari maarufu vijana wa Genz na kuepukana na upotoshaji kupitia mitandao. “Kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia, vijana wengi wamehamia kwenye mitandao ya kijamii, ili kuongeza wigo sasa tumeamua kuwafuata huko na kuanzisha mijadala ya wazi ya elimu ya afya kupitia Tiktok hivyo wanapata wasaa wa kuuliza maswali na kup…