WAZIRI WA FEDHA AITAKA TADB KUWEKEZA ZAIDI KATIKA KILIMO CHA MAZAO YENYE THAMANI KUBWA
WAZIRI WA FEDHA AITAKA TADB KUWEKEZA ZAIDI KATIKA KILIMO CHA MAZAO YENYE THAMANI KUBWA
Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb.), ameielekeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuelekeza mipango na mikakati yake zaidi katika kuendeleza kilimo cha mazao ya chakula na biashara yenye thamani kubwa katika soko la kimataifa, ili kuongeza kipato cha wakulima, wafugaji na wavuvi pamoja na kukuza mchango wa sekta hizo katika uchumi wa taifa. Aidha, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika mazao ya misitu ikiwemo ufugaji wa nyuki, akieleza kuwa sekta hiyo ina fursa kubwa ya kiuchumi na mchango katika uhifadhi wa mazingira na maendeleo endelevu. Ushauri huo umetolewa leo, Februari 1, 2026, Jijini Dodoma, wakati Waziri wa Fedha alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege, ambapo pia alipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Benki hiyo. Katika mazungumzo hayo, Balozi Omar ameahidi kuwa Serikali itae…