ULEGA AAGIZA UCHUNGUZI BILIONI 9.15 ZA MKANDARASI WA KICHINA, ATOA SIKU 28 KUSITISHA MKATABA WA BARABARA YA KYERWA–OMURUSHAKA

ULEGA AAGIZA UCHUNGUZI BILIONI 9.15 ZA MKANDARASI WA KICHINA, ATOA SIKU 28 KUSITISHA MKATABA WA BARABARA YA KYERWA–OMURUSHAKA
Na Diana Byera, Kagera. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu matumizi ya shilingi bilioni 9.15 zilizolipwa kwa mkandarasi wa Kampuni ya Kichina, Shandong Luqiao Co. Ltd, kama malipo ya awali (advance payment) kwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyerwa–Omurushaka, baada ya mradi huo kukwama. Aidha, Waziri Ulega ametoa siku 28 kwa Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Kagera kuhakikisha taratibu zote za kusitisha mkataba na kumfukuza mkandarasi huyo zinakamilika, kutokana na kushindwa kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo ya kilomita 50 kwa kiwango cha lami. Akizungumza katika mkutano uliohusisha viongozi wa serikali, TANROADS, mkandarasi na wananchi wa eneo hilo, Waziri Ulega alisema Serikali iliamua kutekeleza mradi huo kama mkakati wa kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya za Kyerwa na Karagwe, lakini lengo hilo halijafikiwa kutokana na uzembe wa mkandarasi. “Serikali haiwezi kuendelea kuvumilia wakandarasi …