SUNGAMILE YATOA OMBI KWA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAWASILIANO SUNGAMILE, KAHAMA
SUNGAMILE YATOA OMBI KWA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAWASILIANO SUNGAMILE, KAHAMA Kijiji cha Sungamile kilichopo Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ni miongoni mwa vijiji vinavyokumbwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti. Licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuimarisha miundombinu ya mawasiliano nchini, hali bado ni ngumu kwa wakazi wa Sungamile ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi bila mawasiliano ya uhakika. Changamoto hii imekuwa ni adha ya kudumu kwa wananchi, kiasi cha kuathiri kwa kiwango kikubwa maisha yao ya kila siku, shughuli za kiuchumi, huduma za kijamii pamoja na usalama wa kijiji kwa ujumla. Mawasiliano, ambayo kwa sasa ni hitaji la msingi katika maendeleo ya jamii, yameendelea kuwa ndoto kwa wakazi wa Sungamile. Kwa sasa, ili kupata mawasiliano ya simu, wananchi wa Sungamile hulazimika kufanya mambo yasiyo ya kawaida. Ni jambo la kawaida kuona vijana, wazee na hata akina mama wakipanda juu ya miti, kusimama juu ya barabara ya lami au kupanda sehemu za juu zilizo pembezoni mwa kijiji wakijar…