MZUMBE, WIZARA YA FEDHA NA BENKI YA DUNIA KUIMARISHA UNUNUZI WA MIRADI YA MAENDELEO

MZUMBE, WIZARA YA FEDHA NA BENKI YA DUNIA KUIMARISHA UNUNUZI WA MIRADI YA MAENDELEO
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam, kimefungua rasmi mafunzo ya kujenga uwezo kwa taasisi mbalimbali za serikali zinazotekeleza miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, yakilenga kuboresha mchakato wa ununuzi katika miradi ya maendeleo. Mafunzo hayo ni sehemu ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia, yakiwa na lengo kuu la kuongeza ufanisi, uwazi na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Akizungumza leo Februari 2, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa William Mwegoha, amesema mafunzo hayo yatadumu kwa muda wa wiki mbili na yatawahusisha wataalamu kutoka sekta ya serikali na taasisi za umma wanaoshiriki katika utekelezaji wa miradi ya Benki ya Dunia. Profesa Mwegoha amesema ni muhimu kuwajengea uwezo wataalamu wa ununuzi ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufanisi, kwa wakati, na kwa kuzingatia sheria …