Hafla ya uzinduzi wa Mashindano makubwa ya Qur-an Tukufu kwa Mabara yote Ulimwenguni

Hafla ya uzinduzi wa Mashindano makubwa ya Qur-an Tukufu kwa Mabara yote Ulimwenguni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na waumini  wa Dini ya kiislamu katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano makubwa ya Qur-an Tukufu kwa Mabara yote Ulimwenguni kwa mwaka 2026 yanayoandaliwa na Taasisi ya Al-hikman Foundation katika Ukumbi wa Hoteli ya Kilimnjaro Dar es Salaam. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Taasisi ya Al-hikman Foundation kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kueneza ya Dini ya Kiislamu kwa misingi ya elimu, hekima na maadili mema. Ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa mashindano makubwa ya Qur-an tukufu kwa mabara yote Ulimwenguni kwa mwaka 2026 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kilimnjaro jijini Dar es Salaam. Amesema ni jambo la faraja kuona Taasisi ya Al-hikman Foundation inatoa huduma mbali mbali za kijamii zinazogusa maisha ya watu bila ya kubagua dini wala kabila wakiamini kuwa binaadamu wote ni sawa na wanastahiki kupatiwa huduma kwa haki na usawa. Makamu wa Pili wa Rais wa …