DKT. MSEMWA: UTEKELEZAJI WA DIRA 2050 KUANZA JULAI 1, 2026
DKT. MSEMWA: UTEKELEZAJI WA DIRA 2050 KUANZA JULAI 1, 2026 Na Meleka Kulwa – Fullshangwe Blog, Dodoma Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Dkt. Fred Msemwa, amesema kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utaanza rasmi Julai 1, 2026 ukiwa na lengo la kuhakikisha ustawi wa kila Mtanzania bila kujali hali yake. Aidha amebainisha kuwa dira hiyo inalenga kuimarisha mshikamano wa kitaifa na ushiriki wa wananchi wote katika maendeleo ya Taifa huku ikisisitiza kutomuacha nyuma Mtanzania yeyote. Dkt. Msemwa ameyabainisha hayo Februari 01, 2026 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua za maandalizi ya kuanza kwa utekelezaji wa Dira 2050. Amesema kuwa Dira 2050 ilizinduliwa Julai 17, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na baadaye Serikali kuielekeza NPC kuandaa mipango ya utekelezaji wake ikiwemo Mpango Elekezi wa Muda Mrefu wa Miaka 25 (2026/2027–2050/2051), Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2026/2027–2030/2031) pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa w…