CHANGAMOTO YA MAJI KIJIJI CHA SUNGAMILE: BOMBA LA MAJI YA ZIWA VICTORIA LIMEPITA, LAKINI WANANCHI BADO HAWANA MAJI

Maji ni rasilimali muhimu na ya msingi kwa maisha ya binadamu, afya ya jamii na maendeleo ya kiuchumi. Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maji, ikiwemo miradi ya kuchota maji kutoka Ziwa Victoria ili kuwahudumia wananchi wa maeneo mbalimbali.  Hata hivyo, bado zipo jamii zinazoshuhudia miradi hii ikipita karibu au ndani ya maeneo yao bila wao kunufaika, hali inayosababisha maswali na kilio kikubwa kwa wananchi. Kijiji cha Sungamile ni mfano halisi wa hali hiyo. Ingawa Sungamile kiko mbali na Ziwa Victoria, bomba kuu la maji ya Ziwa Victoria limepita moja kwa moja ndani ya kijiji, lakini kwa masikitiko makubwa, maji hayo hayajatolewa kwa matumizi ya wananchi wa Sungamile. Bomba hilo limekuwa kama alama ya matumaini yaliyokatika, kwani wananchi wanaliona kila siku lakini hawawezi kulipata hata tone moja la maji Kwa sasa, wakazi wa Sungamile wanaendelea kukabiliwa na uhaba mkubwa wa maji safi na salama.  Wananchi wanalazimika kutegemea vyanzo duni vya maji kama…