BIBI CLOTILDA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUOKOA MAISHA YAKE

BIBI CLOTILDA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUOKOA MAISHA YAKE
Na OWM - TAMISEMI, Dodoma Bibi Clotilda Isidory Kokupima, mkazi wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, amemtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, na kumuomba awasilishe shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa msaada alioutoa wa Shilingi Milioni 20 kugharamia matibabu ya ugonjwa wa kansa ya utumbo uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu. Akizungumza na Prof. Shemdoe ofisini kwake, Bibi Clotilda amesema alifika ofisini hapo mahsusi kuomba shukrani zake ziwasilishwe kwa Mheshimiwa Rais, ambaye msaada wake ulimwezesha kupata matibabu katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, hatua iliyookoa maisha yake. “Ninamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuokoa maisha yangu. Nilikuwa nikisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya utumbo kwa kipindi cha miaka sita, na matibabu yalisimama baada ya familia yangu kushindwa kumudu gharama. Hata hivyo, baada ya kupata msaada wa Shilingi M…