Yanga Kukutana na Al Ahly Jumamosi Zanzibar, Polisi Waahidi Ulinzi Mkali

Yanga Kukutana na Al Ahly Jumamosi Zanzibar, Polisi Waahidi Ulinzi Mkali
Na Mwandishi Wetu MASHABIKI wa soka nchini Tanzania wanatarajiwa kushuhudia mchezo mkubwa wa kimataifa siku ya Jumamosi, tarehe 31 Januari 2026, ambapo klabu ya Young Africans SC (Yanga) itavaana na mabingwa wa kihistoria wa Afrika, Al Ahly ya Misri, katika mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF). Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 10:00 jioni, ukiwa ni miongoni mwa michezo inayobeba hadhi kubwa barani Afrika kutokana na historia na ubora wa timu hizo mbili. Kuelekea mchezo huo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama limetangaza kuimarisha ulinzi kabla, wakati na baada ya mchezo huo ili kuhakikisha usalama na amani vinaendelea kutawala. Jeshi la Polisi limetambua kuwa mchezo huo ni wa kimataifa na ni fursa muhimu ya kuitangaza na kujenga heshima ya Taifa, hivyo limeahidi kusimamia kikamilifu hali ya usalama ili kuzuia vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani. Kupitia taarifa iliyotole…