WAZIRI PROF. RIZIKI SHEMDOE ATOA MAAGIZO KWA MIKOA TANZANIA BARA
WAZIRI PROF. RIZIKI SHEMDOE ATOA MAAGIZO KWA MIKOA TANZANIA BARA Januari 31,2026 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI )Profesa Riziki Shemdoe, ametoa maagizo kwa mikoa Tanzania Bara kuanza kujipanga mapema kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu, ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ifikapo mwaka 2028. Amesema kuanzia mwaka 2028, wanafunzi wa Darasa la Sita na la Saba watajiunga na Kidato cha kwanza kufuatia mabadiliko ya mitaala, hivyo halmashauri na mikoa zinapaswa kuanza kutenga bajeti mapema ili kuepuka changamoto zitakazoweza kujitokeza baadaye. Ametoa maagizo hayo Januari 31, 2026, wakati wa ziara ya siku moja wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo pia ameelekeza watumishi wapya wa sekta ya Afya na Elimu waliopokelewa nchini kupangiwa vituo kulingana na mahitaji halisi, hasa katika shule zenye uhaba wa walimu na vituo vipya vya afya visivyo na watumishi wa kutosha. Aidha, Prof. Shemdoe amesisitiza viongozi wa wilaya na mikoa kutenga muda wa kusikiliza na ku…