WAZIRI MKUU ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA *Lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia kuhamasisha utalii
WAZIRI MKUU ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA *Lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia kuhamasisha utalii
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumamosi, Januari 31, 2026 ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha utalii. Waziri Mkuu amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amekuwa mstari wa mbele katika kuviuza vivutio vyetu vya utalii duniani kote, sote ni mashahidi namna alivyoshiriki filamu za Tanzania The Royal Tour na The Amazing Tanzania ambazo zimechochea kuitangaza Tanzania na vivutio vyetu kimataifa.” “…Na ndiyo maana na mimi nimepata msukumo wa leo kuja hapa kujionea vivutio vyenu kama sehemu ya kumuunga mkono kwa jitihada zake hizo.” Akiwa katika hifadhi hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zake za uhifadhi kuendelea kutunza mazingira ya hifadhi mbalimbali nchini ili ziwe endelevu. Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kujitokeza kwa …