WAWILI WAFUNGWA MIAKA 30 KWA UBAKAJI

WAWILI WAFUNGWA MIAKA 30 KWA UBAKAJI
Na Mwandishi wetu, Simanjiro WAKAZI wawili wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kumbaka kwa zamu msichana mwenye umri wa miaka 24. Pamoja na kumbaka na kumwingilia kinyume cha maumbile msichana huyo pia walimpora simu aina ya Samsung na kumwibia fedha zake Sh70,000. Hata hivyo, katika hukumu ya kesi hiyo namba 10374/2025 iliyotolewa mji mdogo wa Orkesumet na hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo Nicodemo washtakiwa watatu kati ya watano hawakuwepo mahakama hapo. Hakimu Nicodemo amewataja washtakiwa Meshack Paulo (23) na Ibrahim Ibu (24) ambao ni wachimbaji wa madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani walimbaka, kumlawiti. Amesema washtakiwa hao na wenzao watatu Februari 4, 2025 kwa pamoja walimbaka msichana huyo ambaye ni muhudumu wa bar ya Feri mwenye umri wa miaka 24. Ameeleza kwamba wakati msichana huyo usiku huo wa saa 8 akitoka kazini akitembea kwenda nyumbani alimuona mshtakiwa wa kwanza Meshack akiwa na pikipiki kisha akam…