Waathirika wa Maandamano 29 October 2025 Kupatiwa Matibabu ya Kisaikolojia na Tume
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imetangaza mpango maalum wa kuwapatia waathirika wote wa vurugu hizo huduma ya kisaikolojia. Hayo yamesemwa jana wakati tume hiyo ikiendelea kuchunguza Hatua hiyo imekuja kufuatia mashuhuda na waathirika wengi waliojitokeza kutoa ushahidi wao kuonekana kuwa na makovu mazito ya kihisia na msongo wa mawazo uliokithiri. Mwenyekiti wa Tume hiyo amebainisha kuwa, wakati uchunguzi wa kisheria na utafutaji wa haki ukiendelea, ni jukumu la Tume kuhakikisha kuwa hali ya kiakili ya waathirika inaimarishwa. Alieleza kuwa madhila yaliyowapata wananchi hao ni makubwa na yanahitaji uingiliaji wa kitaalamu ili kuwasaidia kurejea katika hali zao za kawaida na kuendelea na ujenzi wa taifa. Katika vikao vya kusikiliza ushahidi vilivyoanza hivi karibuni, Tume imepokea simulizi za kusikitisha kutoka kwa waathiriwa waliofika mbele yake. Miongoni mwao ni watu waliojeruhiwa kwa risasi, ambapo baadhi yao bado wana…