TANZANIA YANADI VIVUTIO VYAKE MAONESHO YA FITUR NCHINI HISPANIA

TANZANIA YANADI VIVUTIO VYAKE MAONESHO YA FITUR NCHINI HISPANIA
Nchi ya Tanzania imeendelea kunadi vivutio vyake katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii FITUR( Feria Internacional de Turismo) yanayofanyika katika Kituo cha Maonesho cha IFEMA, jijini Madrid, Hispania. Maonesho hayo yameanza Leo rasmi tarehe 21 Januari 2026. Maonesho ya FITUR yanayofanyika jijini Madrid, Hispania, yanalenga kuwa jukwaa kuu la kimataifa kwa sekta ya utalii duniani. Maonesho hayo yanajikita katika kukuza biashara za utalii, kuhamasisha ubunifu na matumizi ya teknolojia za kidijitali, pamoja na kuendeleza misingi ya utalii endelevu unaozingatia mazingira na jamii. Aidha Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ni miongoni mwa taasisi linalotumia jukwaa hilo muhimu linalowakutanisha zaidi ya wadau wa sekta ya utalii mia tano (500) duniani kutangaza Hifadhi za Taifa za Tanzania katika soko la kimataifa, kuonesha vivutio vya kipekee ikiwemo wanyamapori, mandhari na utalii wa, pamoja na kuhamasisha fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana ndani ya hifadhi hizo. Kupiti…