TANZANIA NA MAREKANI KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MADINI
TANZANIA NA MAREKANI KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MADINI ▪️Lengo ni kuongeza eneo la utafiti wa kina wa Madini ▪️Matokeo ya Utafiti kuibua migodi mipya ya kinywe nchini ▪️Tanzania yaainisha mikakati ya kuongeza uzalishaji madini kinywe ▪️Marekani kuwajengea uwezo wa matumizi sahihi ya teknolojia wataalamu wa Tanzania *Dodoma* Serikali ya Tanzania na Marekani zimeendelea kuimarisha ushirikiano wa kikazi katika sekta ya madini, hususan kwenye utafiti wa kina wa madini ya kimkakati yakiwemo madini ya kinywe, kwa lengo la kuimarisha usimamizi, tija, ajira na mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa. Akizungumza leo Januari 21, 2025 jijini Dodoma wakati wa kikao kilichohusisha ujumbe maalum kutoka Ubalozi wa Marekani ulioongozwa na Mhe. Andrew Lentz, Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini pamoja na wataalamu wa Wizara ya Madini, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema ushirikiano huo unatekelezwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini ya Marekani (US Department of States Enegry and Mineral Governance Program) na unalenga kuinua uwezo wa kitaifa k…