‎SERIKALI YAENDELEA KUWASHIKA MKONO WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU

‎SERIKALI YAENDELEA KUWASHIKA MKONO WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU
‎Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Dodoma  ‎Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza ahadi za Rais Samia kwa vitendo, hususan katika kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wanajisikia kuwa sehemu ya jamii na hawatengeki na wanafunzi wengine. ‎Akizungumza na waandishi wa Habari Januari 31, 2026 katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jijini Dodoma, katika kutoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi za Rais samia ndani ya siku 100. ‎amesema kuwa Wizara imenunua na kusambaza vifaa vya kidijiti na saidizi vyenye thamani ya shilingi bilioni 5.4 kwa ajili ya walimu wa shule za msingi na sekondari, wakufunzi pamoja na walimu tarajali wenye ulemavu katika vyuo vya ualimu nchini, kwa lengo la kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji. ‎Amebainisha kuwa jumla ya wanufaika 1,055 kutoka Halmashauri 104 nchini wamenufaika na mpango huo. Amesema kuwa vifaa vilivyosambazwa ni pamoja na kompyuta mpaka…