NDEJEMBI: GHARAMA ZA UMEME HAZIJAPANDA KWA MIAKA 10
NDEJEMBI: GHARAMA ZA UMEME HAZIJAPANDA KWA MIAKA 10 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, akizungumza katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Kumbi za Bunge Jijini Dodoma.Kikao hicho kilihusu uwasilishaji wa taarifa kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuhusu muundo na majukumu ya taasisi hizo. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Saidy. …….. 📌Lengo ni Wananchi wamudu gharama za matumizi ya umeme. Dodoma Licha ya kuongezeka kwa gharama za vifaa vya umeme ikiwemo nguzo, waya na mita, Serikali imeendelea kuhakikisha gharama za matumizi ya umeme kwa wananchi hazipandi kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2016. Akizungumza Januari 21, 2026 jijini Dodoma katika kikao cha pili kati ya Wizara ya Nishati, taasisi zake na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema hatua hiyo imelenga kila mwananch…