MKURUGENZI MKUU WA NSSF AONGOZA UTOAJI WA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KATIKA SOKO LA TEGETA NYUKI
MKURUGENZI MKUU WA NSSF AONGOZA UTOAJI WA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KATIKA SOKO LA TEGETA NYUKI
Na Mwandishi Wetu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba, amesema hakuna sababu kwa mwananchi aliyejiajiri kushindwa kujiunga na Mfuko huo kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa ambayo yanawawezesha kunufaika na mafao mbalimbali sawa na waajiriwa wa sekta ya umma na binafsi. Bw. Mshomba alitoa kauli hiyo wakati alipowaongoza wafanyakazi wa NSSF kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na kuandikisha wanachama wapya katika soko la Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, kupitia kampeni ya NSSF Staa wa Mchezo Paka Rangi. Alisema mwananchi atakayejiajiri na kujiunga na NSSF atanufaika na mafao ya pensheni ya uzeeni, urithi, ulemavu, uzazi, matibabu pamoja na mafao mengine ambayo awali hayakuwa yakipatikana kwa kundi hilo. “Tunaposema wanachama wa NSSF ni mastaa wa mchezo, tunamaanisha kuwa Mfuko unatoa uhakika wa maisha bora, matibabu na kipato hata pale mwanachama anapostaafu. Endapo mwanachama atafariki, wategemezi wake watanufaika na mafao ya urithi,” ali…