MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA JIJINI TANGA FURSA KWA WANANCHI
MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA JIJINI TANGA FURSA KWA WANANCHI
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa na Timu ya Uratibu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kutoka Wizara ya Fedha katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jiji la Tanga kuhusu maadhimisho ya tano ya ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu Na Eva Ngowi na Chedaiwe Msuya, WF, Tanga Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema, pamoja na timu ya uratibu, wamefanya majadiliano na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba, kujadili kuhusu Maadhimisho ya Tano ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyoanza jana na yatazinduliwa rasmi kesho katika viwanja vya Usagara Jijini Tanga. Majadiliano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa…