KATA ZA MZINGA, MALANGALI KUPIGA KURA KUCHAGUA MADIWANI

 Dodoma ‎Jumla ya Wapiga Kura 38,151 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki katika uchaguzi wa marudio katika Kata za Malangali iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa na Mzinga iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. ‎Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amesema hayo leo Januari 21, 2026 jijini Ddodoma wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika Kata hizo utakao fanyika Januari 22, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 92 vya Kupigia Kura vitatumika. ‎Aidha, amesema jumla ya wagombea sita (6) kutoka katika vyama vya siasa vitatu (3) wanawania nafasi wazi za udiwani katika maeneo hayo na kuvipongeza vyama vya siasa na wagombea waliojitokeza kushiriki katika uchaguzi huo.  ‎“Kati ya wagombea sita (06), wagombea watano (05) sawa na asilimia 83.3 ni wanaume na mgombea mmoja (01) sawa na asilimia 16.7 ni Mwanamke. Kwa namna ya pekee, Tume inavipongeza vyama vilivyoshiriki na wagomb…