KAMATI YA MIUNDOMBINU YASISITIZA KIPAUMBELE KWA WAKANDARASI WAZAWA

KAMATI YA MIUNDOMBINU YASISITIZA KIPAUMBELE KWA WAKANDARASI WAZAWA
…….. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeisisitiza Wizara ya Ujenzi kuendelea na mkakati wa kuinua na kuwasaidia Makandarasi wazawa ili kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa miradi ya mbalimbali ya ujenzi nchini. ‎Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso leo Januari 21, 2026 mara baada ya kupokea taarifa ya Wizara ya Ujenzi kuhusu muundo, majukumu pamoja na Sera na Sheria zinazotekelezwa na Wizara hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega mbele ya kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma. ‎”Wekeni mazingira mazuri ya kuwasaidia makandarasi wa ndani, ongezen fursa mbalimbali za miradi, walipwe kwa wakati kwani mkifanya hivi mtasaidia ufanikishaji wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi nchini na kusaidia kukuza uchumi wa nchi”, amesema Kakoso. ‎Aidha, Kakoso ametoa rai kwa Wizara hiyo kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kushirikiana na Sekta Binafsi (PPP) ili Wizara kupata wigo na fursa ya kutekeleza miradi mingi zaidi kupitia mfumo huo. ‎Kwa upande wa…