HALMASHAURI KUU YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KISHAPU, ASILIMIA 48.9 YAFIKIWA NDANI YA MIEZI SITA

HALMASHAURI KUU YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KISHAPU, ASILIMIA 48.9 YAFIKIWA NDANI YA MIEZI SITA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Shija Ntelezu akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya kishapu cha kupokea taarifa ya Wilaya ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama hicho Wilaya ya Kishapu Januari,21,2025 Na Sumai Salum – Kishapu Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imeendelea kuonesha mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025, baada ya kufikia asilimia 48.9 ya utekelezaji katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2025. Taarifa hiyo imewasilishwa Januari 21, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama hicho Wilaya ya Kishapu. Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu …