DKT. KILABUKO AZINDUA NYARAKA ZA USIMAMIZI WA MAAFA NKASI
DKT. KILABUKO AZINDUA NYARAKA ZA USIMAMIZI WA MAAFA NKASI
NA.MWANDISHI WETU – NKASI Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. James Kilabuko amezindua nyaraka za usimamizi wa maafa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa huku akisisistiza nyaraka hizo kutekelezwa kwa vitendo. Dkt. Kilabuko amesema hayo leo 27 Januari, 2026 wakati wa uzinduzi huo na kusema kuwa, hatua hiyo ni mwanzo wa kuanza kazi rasmi endapo kutatokea janga lolote, na kutoa wito kwa idara, vitengo na taasisi ngazi ya wilaya kuzingatia nyaraka hizo kwa kuhakikisha zinakuwa chachu ya kuongeza ushirikishwaji wa jamii na wadau katika masuala ya menejimenti ya maafa. Ameongeza kuwa, hatua hiyo itasaidia kujenga uelewa wa jamii kuhusu masuala ya usimamizi wa maafa, kuimarisha mfumo wa utoaji wa tahadhari awali, kujenga uwezo wa kuzuia, kupunguza madhara na kujiandaa na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea. Dkt. Kilabuko alifafanua kuwa, nyaraka hizo zimekuja wakati sahihi kwa kuzingatia kuwa, Wilaya imekuwa ikikabiliwa na maafa ya…