BARAZA LA WAFANYAKAZI LAJADILI RASIMU YA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA 2026/2027
BARAZA LA WAFANYAKAZI LAJADILI RASIMU YA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA 2026/2027 ……. Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma limekutana kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za halmashauri pamoja na rasimu ya mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo uongozi huo ulieleza kiasi cha bajeti kinachotarajiwa kutekelezwa katika kipindi hicho. Akizungumza katika kikao hicho, Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Francis Kaunda alisema kuwa halmashauri imekasimia kukusanya shilingi bilioni 166 kutoka vyanzo vyake vya ndani, serikali kuu na wahisani mbalimbali kwaajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo, utoaji huduma na kujiendesha. Kaunda alisema kuwa kutoka mapato ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 73 kinatarajiwa kukusanywa ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 46 ni mapato yasiyolindwa na shilingi bilioni 27 ni mapato lindwa. Fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida. Aliongeza kuwa kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 32 kimepangwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo…